UKOSOAJI WA POLISI KWA KAZI YAO.

Kazi wanaoifanya polisi wa humu nchini kamwe kwa upande mwingine huwezi kuishabikia kwa anyeona ipo kazi shwari kwa vitengo vyao.Ndio maana naweza kusema,”kazi inayofanywa na kitambulisho hudumu kwa muda mfupi, lakini utambuzi kutoka kwa kazi hudumu kwa muda mrefu”. Wanasiasa kila wapitapo linalotoka kinywani mwao ni kwamba vijana wanaumia, kwa kweli sisi vijana hatuna bahati humu nchini. Wanasiasa wataimba huu wimbo wa kinyume eti vijana wasaidiwe huku tukiangamia.

Sehemu zote Kenya iwe vijijini iwe katika jiji kuu, polisi wameanza”kulawiti” Vijana jina hili kulawiti usilichukulie kikawaida, hapana! Eti kulawiti ni kule kwa wanawake blabla hamna jina hili lina uzito mkubwa ukifungua macho na akili yako. Polisi walio vijijini ama mahala popote kule, wanalia na kuomba waletwe jijini Nairobi. Hivi majuzi, nimekaa kwa kikao cha wanapolisi na waliyoyazungumza bila shaka nilijuta kukaa nao. Mwingine akilia apewe rufaa aende Nairobi mwanzo Nairobi pesa za hongo zipo kwa wingi. Nakubaliana na suala lake na ombi lake kutumwa Nairobi, askari siku hizi hawangalii Mshahara wao wanachoangalia ni hongo. 
 
Hii leo hapa huwa mtu akifanya kazi iwe nzuri ama mbaya, nzuri ndio husifiwa nayo mimi naenda moja kwa moja hadi ile mbaya ya askari. Askari badala wafanye kazi shwari, kazi yao ni kuwakamata vijana wakiwa kwenye pilkapilka zao, hata bila kosa kusudi tu wapewe rushwa na kuwaachilia. Hii ndio maana nasema vijana wamekua kitega uchumi kwa  polisi mwanzo vijana wakikamatwa njiani, wanatishiwa kutoa kitu kidogo ndio waachiliwe na iwapo huna elfu moja huwezi kuachiliwa kamwe hadi kwenye kituo chao. Ukifika ndani wanaona huna pesa wanadanganya na kukubadilishia kesi, wanasema ulikua ukipora watu jijini ama ulikua unapanga kikundi cha ugaidi. Walivyosema wazungu,”A leader is always right” watu wawili humu duniani, mimi naogopa sana Mwalimu na Askari. Hawa wawili watakachokisema ndio uamuzi. Askari wanawasaliti vijana kwani wao wanataka kujitajirisha ndio maana nasema kila kuchao kila mtu anaomba Mungu ampe maisha marefu.
 
Jiji la Nairobi na vijana wanaoishi humo, sasa hivi vijana hawana la ziada wakikamatwa ni kusalimu amri na kukubali, mimi sisemi hili kwa serikali kufanya juhudi kuwaokoa vijana mwanzo umekua ni wimbo. Askari wanauamuzi wa kuwaonea vijana maskini huruma na kuwaacha wadensi humu duniani bila mawazo. Ndio maana naweza sema  usipofuta kibao kamwe hutoelewa kwanini gari la kubeba taka nalo hupelekwa”Car wash”likaoshwe ili likabebe taka, tena hivi una maana gani Mungu akupe maisha marefu alafu kila siku upoteze muda tu, yaani unaomba Mungu akupe maisha marefu, mali, utajiri na cheo ili ukifanikiwa utunyanyase.
 
Mimi kwa sasa siwezi kusifu kituo chochote cha askari humu Nchini eti kazi wanaoifanya ni nzuri wala mbaya, askari hukumu yaja na kumbuka nawe una mtoto mahali amabaye yupo sawa na watoto wa wenzio. Bila shaka waliosema tenda wema nenda zako nawapa mkono wa buriani walipo wawe na siha za moyo. Ndio maana pia nawezasema ikiwa unataka kitu kutoka mayoni basi inachukua kazi nzima kukutambulisha.
 
Journalism Student & Aspirant President of the Student Council/ Union

1 comment

  • / Reply

    Hello there! I just want to give you a huge thumbs up for your great information you have got here on this post. I will be coming back to your website for more soon.| Yolane Stanfield Clarie

Leave a comment

× Chat With Us Now