MCHAKATO WA BBI

Mchakato huu unaongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga, ulianza na safari ya ya kisii ulipofika kule katika kaunti ya kisii aliyepewa kuwa mwenyekiti ni Juneth Mohammed. Magavana woote wa nyanza wameungana kuunga mkona BBI. Alipopewa nafasi mbunge wa borabu Ben Momanyi alisema kwamba ingewezekana referendum kufanyika jioni hiyo baada ya mkutano wa kisii kuisha kwa upande wa kinara wa ODM Raila Odinga alisema kwamba watu Wa nyanza ikiwemo waluo, wakuria, wakisii waungane na kuunga Mjakato huu mkono aliongeza kwamba msafara wa BBI umehakikisha umejengwa na kutekeleza, pia alisema kwamba wananchi wameamua Kenya iwe na mwanzo mpya alizidisha zaidi eti kuna America revolution Uingereza, uchina misri nchi hizi zote Zina revolution. Swali langu ni je yaani is a must we compete with other nations let’s do our only plans and we Wil succeed tuache kutegemea nchi zingine na tujitegemee sisi. Alisema kwamba Vijana wa humu nchini Wana changamoto chungu nzima na wanastahili kuibadilisha Kenya aghalabu kuwa boraheri, alisisitiza kwamba Kenya Hali si bora kweli, vile vile swali langu kwa Raila Odinga ni je tangu aanze kubadisha nchi hi ya kenya hajatosheka mwanzo akibadilisha Tena baadae anakuja anasema vitu si bora kamwe. Kwa upande wangu mbona wanasiasa wanaamua kuzungumzia wananchi wamekubali kuibadilisha nchi hii makala haya nmeyaona Mara si moja, pendekezo langu kwa BBI ni kuwa wanapopitakaunti baada ya nyingine napendelea wawe wakiwapa wanakaunti kipasa sauti aghalabu kutoa Hoja zao kuhusu Mchakato huu.

 
MCHAKATO WA KAKAMEGA
 
 Bila shaka BBI inausisha magavana wanaomaliza hatamu zao za uongozi hasua wale wako katika muhula wa pili, swali langu ni je mbona wasitulie na kufanyia wananchi kazi, mbona magavana Hawa wasiandae safari na msafara wa kutembea katika vitongoji  humu nchini na kuwasaidia Vijana. Hawa wote wanaotembea ukweli uliopo Hawa watu wote ni wazee na mababu zetu mzee kama Atwoli sjui ntamwitaje mwanzo ni mzee wa karne. Hakuna mwana kaunti wa kakamega Ata mmoja alisimama kuzungumzia suala hili la BBI, Kenya kwa Sasa ina Rais ambaye naweza Sema ni kijana kwa upande wangu, anafa kuweka Vijana katika utendakazi wake, Kenya hii hakuna aliyekuwa mzuri kamwe Atwoli alisema kwamba Ruto ana pesa za wizi, swali langu ni je iwapo Ruto ni mwizi na Atwoli Ana kila sababu ya kusema Ruto ni mwizi mbona asiende koti na kuamuaru Ruto akamatwe, Raila akiwa kisii alisema kwamba BBI inasaidia Vijana, na Atwoli akasema inasaidia Vijana wakenya je Musalia mudavadi na Moses wetangula ni Vijana mwanzo alisema BBI itasaidia Wetangula na Mudavadi juu itawasaidia kupata viti vya juu uongozini Haki ya mama hakuna aliyekamilika Kenya hii na Vijana wengi wataendelea kuteseka.
BBI hii inalenga wazee waliokatika nyadhifa za uongozi na kuwatetea waendelee kuongoza huku Vijana waliochini wakiiangaika, Atwoli alisema eti alisaidia vijana wengi Musalia mudavadi, omboko milemba aliwasaidia. Atwoli ni mwenye hela Sasa ni billionaire, Nina uhakika kijiji Atwoli alizaliwa na kulelewa Kuna watu wazima na vijana wasiojiweza mbona anamwita Moses wetangula kijana. Kwa upande wangu Sina furaha na sipendezwi na michakato hii ya BBI mwanza inalenga wazee waliokolea miaka  na wako uongozini ndo wanaelekea kufaidika huku wakenya wa kawaida wakiteseka, naomba mungu ashuke mwenyewe aisaiendie nchi yetu ya kenya asitumane.
 
 
 
Bila kujirudia huku na kule mchakato huu unalenga kushawishi kaunti moja zaidi ya nyingine Ata wakiweka mchakato uwe katika nchi mojawapo ya makao ya umoja wa mataifa yaani United Nation chini Uswizi lengo ni lilelile.
Wakenya wenzangu chagueni Kenya iende moja kwa moja referendum ama isalie ivi ivi ilivyo. Katitamati nafika mwisho wa mchakato wa BBI nikiomba na kutarajia wakenya wa kawaida wanajukumu la kujiamualia si wanasiasa kujiamulia. I think Kenyans don’t need any entertainment yet the country is not stable eti nobody can stop reggae Kenya ni reggae inamba ndani ya wakenya ama wanachokifikiria ni Hali ya kujishughulisha na maisha yao. 
 
Na MATHEW OCHACHI
Student: Journalism & Mass-Communication
 

Leave a comment